Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndevu zamponza bondia mashindano ya Taifa

Ndevu+pic Ndevu zamponza bondia mashindano ya Taifa

Wed, 5 Aug 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Imani MakongoroBONDIA Emmanuel Pascal amejikuta akiponzwa na ndevu zake na kumpa ushindi wa chee mpinzani wake, Hussein Juma kwenye mashindano ya ndondi ya taifa yanayoendelea viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe, Dar es Salaam.

Mashindano hayo ya wazi yalifunguliwa jana Jumanne jioni kwa mapambano 10 kupigwa uwanjani hapo, huku bondia huyo akiondoshwa mashindanoni.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ngumi za Wazi Tanzania (OBFT), Lukelo Wililo amesema Pascal alikosa sifa za kupanda ulingoni kutokana na kuachia ndevu kinyume na taratibu za mchezo huo.

"Aliondolewa na kumpa ushindi mpinzani wake ambaye amefuzu kucheza raundi ya pili," amesema Lukelo.

Bondia mwingine, Huled Rashid wa MMJKT alipewa ushindi wa chee raundi ya kwanza baada ya mpinzani wake Mahafudh Abdallah kutoka nje ya mchezo.

"Mahafudh alikuwa akipigana rafu bila kufuata utaratibu kabla ya pambano lake kusitishwa na mpinzani wake kupewa ushindi raundi ya kwanza," amesema Lukelo.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz