Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanasheria amuonya Hassan Mwakinyo

Hassan Mwakinyo Jrrrr Mwanasheria amuonya Hassan Mwakinyo

Wed, 15 Nov 2023 Chanzo: Dar24

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ikielekeza bondia Hassan Mwakinyo kupelekewa wito wa kufika mahakamani kupitia gazeti la Mwananchi kufuatia kesi ya madai inayomkabili, wakili kiongozi wa kampuni ya uwakili ya Haki Kwanza, Alloyce Komba ameeleza kile kinachoweza kumpata kama ataendelea kutotokea mahakamani kusikiliza kesi.

Juzi jumatatu (Novemba 13), kesi hiyo ilitajwa mara ya kwanza na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Amiri Msumi aliyetoa uamuzi wa bondia huyo kupelekewa wito wa kufika mahakamani kupitia gazeti la Mwananchi baada ya kukataa kupokea hati ya wito iliyowasilishwa kwake na msambaza nyaraka wa Mahakama.

Akizungumza kwa muktadha wa kisheria, Komba amesema Mwakinyo hawezi kukwepa kesi hiyo na kama ikitokea hatafika mahakamani, basi upande wa mashtaka utaomba isikilizwe upande mmoja na Mahakama haiwezi kukataa.

“Kupelekewa wito wa kufika mahakamani kupitia gazeti ni samansi mbadala, kama Mwakinyo atakwenda mahakamani Novemba 20, 2023 ili kusikiliza kesi yake itakapotajwa tena, basi itasikilizwa pande zote mbili na kujitetea.

“La sivyo upande wa mdai ukiomba isikilizwe upande mmoja ikileta ushahidi wake (ex parte hearing) ikaamuriwa hivyo, Mwakinyo hatatafutwa tena, matokeo yake ni asubiri hukumu ya upande mmoja (ex parte judgment) huwa ambayo madhara makubwa.

“Mdai akishinda atapata decree (ya kukazia hukumu) anaweza kukamata akaunti za benki au mali zake mdaiwa,” alisema Komba akifafanua kwamba ili kesi isikilizwe pande zote ni upande wa Mwakinyo kufika.

Mwakinyo alifunguliwa kesi ya madai na kampuni ya PAF Promotion ikiwamo kuilipa Sh150 milioni ikiwa ni madhara ya jumla baada ya kutopanda ulingoni tofauti na mkataba aliosaini kwenye pambano la Septemba 29. Bondia huyo awali alidai sababu za kutopigana ni promota kukiuka makubaliano.

Wakili wa PAF Promotion, Herry Kauki alidai walipeleka wito Serikali ya mtaa, lakini Mwakinyo aligomea kupokea wito wa kufika mahakamani.

Chanzo: Dar24