Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwamuzi pambano la Mandonga asimamishwa

Screenshot 20220925 005151 Mandonga Mwamuzi pambano la Mandonga asimamishwa

Tue, 27 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwamuzi Habib 'Mkarafuu' Mohammed aliyechezesha pambano la Karim 'Mandonga' Said na Salim Abeid amesimamishwa.

Mkarafuu ambaye ni Mwenyekiti wa Chama ca waamuzi wa ngumi za Kulipwa nchini ameondolewa kwenye orodha ya waamuzi kwa muda baada ya kukiri kushindwa kumudu kuchezesha pambano hilo lililopigwa Usiku wa kuamkia Jumapili mkoani Mtwara.

Matokeo ya pambano hilo yalifutwa na rais wa Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBRC), Chaurembo Palasa baada ya mwamuzi kuonyesha kutolimudu baada ya Mandonga kupigwa na kudondoka chini lakini hakumhesabia kama kanuni zinavyotaka hadi aliponyanyuka.

Katibu wa Chama cha waamuzi wa ngumi za kulipwa, Emmanuel Mlundwa amesema mwamuzi huyo ametakiwa kurudi darasani kabla ya kuruhusiwa kuendelea na majukumu ulingoni.

Amesema rais wa TPBRC hakukosea kufuta matokeo kwa kuwa kama yangeingizwa kwenye rekodi, mtandao wa ngumi za kulipwa wa dunia (Boxrec) ungehitaji video zake kwanza.

"Hivyo ingeleta mtizamo hasi kwenye ngumi zetu, lakini kama Chama tumejiridhisha kuwa kulikuwa na makosa mengi ya kiuamuzi kwenye pambano hilo, huenda yamechangiwa na waamuzi wetu kukaa muda mrefu bila kushiriki kwenye kozi mbalimbali na ndicho kimetokea kwa Mkarafuu," amesema Mlundwa.

Amesema kutokana na makosa hayo, Chama kimemsimamisha mwamuzi huyo kuchezesha pambano lolote hadi atakaporudi darasani kuongeza ujuzi kwenye kozi za waamuzi miezi miwili ijayo," amesema.

Mwamuzi huyo ameridhia adhabu hiyo na kukiri kushindwa kumudu pambano hilo ambalo alidai uamuzi wake ulitokana na makosa ya kibinadamu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live