Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwakinyo uso kwa uso na bondia wa dunia

Mwakinyo Hassan Mwakinyo uso kwa uso na bondia wa dunia

Fri, 25 Mar 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Bondia Hassan Mwakinyo amekutana kwa mara ya kwanza na kuzungumza na nyota wa zamani wa dunia wa uzani wa middle na light heavy, Bernard Hopkins Jr.

Mwakinyo amekutana na bondia huyo ambaye ni mmoja wa wamiliki wa Golden Boy Promotion inayoandaa mapambano ya ngumi makubwa Marekani.

Hopkins Jr, bingwa wa zamani wa mataji ya dunia ya WBA, IBA, IBF, WBO, WBC na IBO ambaye amewahi kumiliki nyota tano mwenye rekodi ya kushinda mapambano 55, amezungumza naye kwa dakika kadhaa akiwa katika maandalizi kuelekea pambano lake la Aprili.

“Ni miongoni mwa mabondia maarufu ambao nimekutana nao nikiwa huku. Alikuja kwenye gym ambayo najifua na yeye ni miongoni mwa wamiliki wa Golden Boy Promotion,” alisema Mwakinyo.

Hopkins Jr pambano lake la mwisho la ngumi alichapwa na Joe Smith Jr kwa KO ya raundi ya nane na kuvuliwa moja ya mataji yake ya WBC International kabla ya kustaafu na kujitosa kwenye uandaaji wa mapambano.

Mwakinyo yupo Marekani tangu mwanzoni mwa mwezi huu ambapo ana programu ya kucheza mapambano kadhaa kabla ya kuwania ubingwa wa dunia. “Kama nilivyokwishasema niko kwenye maandalizi ya pambano langu la awali la Aprili. Nimejipanga na nimekuwa na programu nzuri ya mazoezi huku ikiwamo ya sparing (mazoezi ya kuzichapa ana kwa hana),” alisema.

Mwakinyo ni bondia namba moja Afrika na wa 14 duniani kwenye uzani wa super welter.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz