Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwakinyo kuzichapa na Mkongo April

Mwakinyo Gloves .jpeg Bondia Hassan Mwakinyo

Sun, 26 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia Hassan Mwakinyo anatarajiwa kupanda ulingoni April 23 mwaka huu kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma kupambana dhidi ya bondia mkongomani Kuvesa Katembo.

Pambano hilo lisilo la ubingwa, linaandaliwa na kampuni ya Lady in Red Promotion iliyo chini ya Mbunge wa viti maalamu mkoa wa Mbeya, Mhe. Sophia Mwakagenda, likilenga kukusanya taulo za kike Kwa wanafunzi wa nyanda za juu Kusini.

Katembo, ambaye Julai 01 mwaka Jana alipoteza Kwa pointi Tanzania dhidi ya Hamis Maya, amecheza mapambano 22 ameshinda 14 amepoteza 7 na sare 1.

Hii ni Kwa mara ya kwanza tangu Septemba 03 mwaka 2021, MWAKINYO anacheza kwenye ardhi ya Tanzania, ambapo pambano hilo la mwisho kucheza Tanzania, alishinda kwa TKO raundi ya 4 dhidi ya Julius Indongo wa Namibia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live