Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwakinyo kuwania mataji mawili kwa mpigo

92971 Pic+mwakinyo Mwakinyo kuwania mataji mawili kwa mpigo

Fri, 24 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

BONDIA namba moja nchini, Hassan Mwakinyo kwa mara ya kwanza atazichapa kuwania mataji mawili kwa mpigo ya ubingwa wa mabara wa WBF na UBO. Mwakinyo atamkabiri, Rodolfo Ezequiel 'Epi Scania' wa Argentina katika pambano litakalopigwa jijini Dar es Salaam kwenye uwanja wa Uhuru, Machi 28 mwaka huu. Kwa mujibu wa promota wa pambano hilo la uzani wa super welter, Ally Mwanzoa, tayari mabondia wote wamesaini mkataba kuzichapa siku hiyo katika pambano lililopewa jina la Usiku wa Mabingwa. Akizungumzia pambano hilo, Mwakinyo alisema limekuja wakati ambao alikuwa akitamani kucheza mapambano ya ubingwa. "Sikuwa nimecheza mapambano ya ubingwa muda mrefu, ili limekuja wakati muafaka, sitofanya makosa," alisema Mwakinyo ambaye amezidiwa uzoefu na mpinzani wake. Rodolfo ameshinda mapambano 44 (16 kwa KO) amepigwa mara 9 (4 kwa KO) na kutoka sare mara tatu wakati Mwakinyo ameshinda mapambano 16 (11 kwa KO), amepigwa mara mbili (moja kwa KO).

Chanzo: mwananchi.co.tz