Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwakinyo awatolea uvivu wanaomponda Dullah Mbabe kupigwa Uingereza

Mwakinyooo Mbabe A0006 Mwakinyo awatolea uvivu wanaomponda Dullah Mbabe kupigwa Uingereza

Thu, 4 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia namba moja Tanzania, Hassan Mwakinyo 'Champez' amewajia juu wanaomkashifu bondia mkongwe, Abdallah Pazi maarufu kama Dullah Mbabe amepoteza pambano lake Kwa knock out (K.O) dhidi ya bondia muingereza Callum Simpson kwenye round ya 4 katika pambano la raundi 10.

"Leo hii watu wengi bila kujua mtu kama Dullah Mbabe ni kwa namna gani? Hautaacha kuzungumzia mchango wake mkubwa kwenye tasnia yetu ya ngumi na katika mema yake aliwahi kushinda nje ya nchi mara mbili kwa kupiga watu KO tena nchi ngumu kama Russia, jambo ambalo kwa viwango vya wachezaji wetu hutokea kwa nadra na bahati mbaya sana tena kutoka karne moja mpaka karne nyengine.

"Wakati huo hakuna aliekuwa proudly na ushindi wake wala kuzungumzia popote pale kama ambavyo leo naona machafuko ya kila aina matusi na kashfa za watu juu yake kuona kama kukosa matokeo kwake ni sehemu ya kufurahisha wengine.

"Anyway pole sana msena wangu wewe ni katika watu naujua mchango wako mkubwa sana kwenye maendeleo ya hatua zangu na bado hakuna siku itafika nikutoe thamani na heshima yako.

"Kibinaadam niseme kwamba ni Mwenyezi Mungu pekee ndio anajua ni kwa nini anakupitisha kwenye haya usikate tamaa kaka hakuna namna utafanikiwa kwa kuepuka maumivu utakayo lazimika kupitia. Achana na mihadarat na makundi ya ajabu fanya kazi," amesema Mwakinyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live