Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwakinyo awataka mabondia wenye 'midomo' wajitokeze

Hassan Mwakinyo Jrrrr Hassan Mwakinyo.

Wed, 12 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkali wa Professional Boxing nchini Tanzania Hassan Mwakinyo "Champez" amewakaribisha mabondia wanaotaka kupambana nae yupo tayari wajitokeze.

"Amerika wanapigana kwasababu wanachezea mikanda mikubwa ambayo kuna wakati inawakutanisha lazima wapigane, hawapigani kwasababu ya kuwekewa chochote.

"Lakini pia wanapigana super rank yani mara nyingi yani mara nyingi ma-boxer wanaopigana mabingwa wanakuwa washakutana mara nyingi mazoezini kwa hiyo anataka kuiaminisha Dunia kuwa flani haniwezi nishampiga mara nyingi mazoezini sasa nampiga uringoni.

"Kwa hiyo kama kuna Boxer yoyote ana hamu ya kupigana namimi achezee mkanda kama huo kwa sababu sio hasara kwangu nimepigana na mtu ambaye yupo ranked.

"Lakini bahati mbaya nasikitika kwamba bado inaweza kuwa ni ndoto ngumu sana kwao kwa sababu moja ya sheria ngumu za ule mkanda.

"Kwa hiyo kwa kujiamini kiume kama mtoto mwenye misuli ya Sokwe, kama kuna Boxer yoyote anaenihitaji kupimana namimi katika uzito wangu, awe mapafu ya panya au yule Ngisi mimi nipo tayari ili tufanye pambano ambalo halitakuwa la ulingoni kushusha heshima yangu.

"Kiasi cha kumtia adabu ili wahakikishe linapotajwa jina la Mwakinyo awepo mmoja wenu ambaye ametia udhu," amesema Mwakinyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live