Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwakinyo atamba kumpiga Kuseva

Bondia Hassan Mwakinyo Bondia Hassan Mwakinyo

Thu, 20 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia Hassan Mwakinyo, amepania kuonyesha kiwango kikubwa dhidi ya Mpinzani wake Kuvesa Katembo kutoka Afrika Kusini kuelekea katika pambano la ‘Night With Purpose’.

Pambano hilo la raundi nane lisilo la ubingwa, limepangwa kufanyika Jumapili (April 23) katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Mwakinyo amesema pamoja na pambano hilo kutokuwa na ubingwa, amejipanga kuhakikisha anamchakaza mpinzani wake ili kubakisha heshima Tanzania.

Bondia huyo amesema amejipanga kumpiga wake mpinzani kuwa, huku akiwaahidi Watanzania kuonesha kiwango bora na kuwapa burudani ya aina yake.

“Nimejipanga kucheza vizuri pia kuonyesha namna gani ngumi inapigwa, Watanzania na mashabiki zangu wategemee kupata burudani nzuri siku hiyo kutoka kwangu,” amesema Mwakinyo.

“Siku hiyo nitacheza kwa heshima kubwa, hivyo mpinzani wangu aje kwa tahadhari kwa sababu nitacheza kwa kiwango kikubwa,” alisema.

Naye Promota pambano hilo, Mbunge wa Viti Mbunge Maalumu, Sophia Mwakagenda, amesema fedha zitakazopatikana katika mpambano huo zitatumika kununua taulo za kike.

Amesema taulo hizo zitagawiwa kwa wasichana katika Iringa, Wanaoishi mikoa ya Njombe, Ruvuma na Mbeya.

Katika hatua nyingine Mwakagenda amesema pambano hilo litanogeshwa na msanii wa singeli, Suleiman Jabir ‘Msaga Sumu’ na mwimbaji wa Bongo Fleva, Khadija Shaban ‘Keisha’.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live