Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwakinyo apigia hesabu ubingwa dunia

90592 Mwakinyo+pic Mwakinyo apigia hesabu ubingwa dunia

Thu, 2 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Baada ya kuporomoka kwa nafasi tatu kwenye viwango vya ngumi duniani, Hassan Mwakinyo amesema atatumia pambano lake la mwezi ujao la ubingwa wa dunia kurudi katika ubora wa kimataifa.

Mwakinyo ameporomoka kutoka nafasi ya 17 hadi ya 20 kwenye viwango vya ngumi za kulipwa duniani katika uzani wa super welter vinavyotolewa na mtandao wa ngumi wa dunia (boxrec).

Bondia huyo wa nyota nne licha ya kuendea kuwa namba moja Afrika katika uzani wa super welter, ameporomoka katika ubora wa dunia huku akieleza sababu ni kutopigana mara kwa mara.

“Mabondia wa nyota tano, nne na nusu mpaka nne kama mimi wako wengi na wanapigana mara kwa mara, wakishinda wanaongeza pointi na kupanda,”alisema Mwakinyo.

Bondia huyo ambaye pambano lake la mwisho alimchapa kwa pointi Arnel Tinampay wa Philippines Novemba, mwaka jana alisema ana matarajio ya kupanda mara zaidi kwenye viwango hivyo mwezi Februari. “Nitacheza pambano la ubingwa wa dunia, naamini litanipandisha mara dufu katika ubora,” alisema bondia huyo namba moja nchini.

Alisema ameanza maandalizi ya pambano hilo ambalo litaadaliwa na promota wake Ally Mwanzoa akiamini atashinda na litamuongezea nyota zaidi kutokana na maandalizi anayofanya.

Chanzo: mwananchi.co.tz