Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwakinyo apania kumchapa Denes

9a862f77bfbfb9f2a77f8e872ecbf44e.png Mwakinyo apania kumchapa Denes

Sun, 28 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

BONDIA wa ngumi za kulipwa Hassan Mwakinyo amesema mazoezi ya nguvu anayofanya kwa muda mrefu yanalenga kufanya vizuri katika pambano lijalo dhidi ya bondia Brendon Denes kutoka Zimbabwe.

Pambano hilo la ubingwa wa Afrika kuwania mkanda wa ABU la raundi 12 linatarajiwa kuchezwa Aprili 9, Dar es Salaam.

Awali, pambano hilo lilikuwa lifanyike Machi 26, lakini likasogezwa mbele baada ya kutokea kwa kifo cha Rais John Magufuli na serikali ilitangaza kuwepo kwa maombolezo ya siku 21.

Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, Mwakinyo alisema anafanya mazoezi ya nguvu kwa sababu hataki kumdharau mpinzani yeyote, bali kujiweka vizuri ili kushinda.

“Mpinzani hata kama ni mdogo huwezi kumdharau ni muhimu kujipanga kwa kujua mashabiki wako wanataka nini, nataka siku zote kushinda kwa sababu nina malengo,” alisema.

Mwakinyo ambaye alianza mazoezi muda mrefu alisema alipata hofu kubwa ya kurudi nyuma baada ya kutokea kwa msiba wa taifa lakini anaamini mambo yatakuwa mazuri.

“Ukweli sikutamani pambano liahirishwe lakini hatukuwa na namna kwa sababu msiba uliotokea ni mkubwa, iliniumiza kwa kuwa nilikuwa nafanya mazoezi ya nguvu na yanauma, naamini mambo yatakwenda vizuri,” alisema.

Chanzo: www.habarileo.co.tz