Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwakinyo apanda viwango vya ubora duniani

FBVbqGNWYAMBBUw Bondia Mtanzania, Hassan Mwakinyo

Mon, 11 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo, amepanda viwango vya ubora katika mchezo wa masumwi kutoka nafasi ya 11 aliyokuwa anaikamata awali na sasa kufikia nafasi ya 10.

Mwakinyo aliepo kwenye uzani wa Super Welter Weight kwa sasa anashika nafasi ya 10 kati ya mabondia 1530 wa uzito huo.

Mwakinyo kwa sasa ana nyota 4, katika upande wa mabondia wa uzito wake na pambano lake la mwisho aliibuka na ushindi dhidi ya Julius Indongo kutoka Namibia.

Katika pambano hilo mwakinyo alishinda kwa TKO raundi ya 4, pambano ambalo lilipigwa katika ukumbi wa Ubungo Plaza Jijini Dar es Salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live