Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwakinyo apagawisha mashabiki Dar, wamuonya Kiduku

Mwakinyo 1 Pic Data Mwakinyo apagawisha mashabiki Dar, wamuonya Kiduku

Sat, 4 Sep 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Ushindi wa Technical Knock Out (TKO) uliwaongezea mzuka mashabiki wa bondia Hassan Mwakinyo usiku wa kuamkia leo huku wakimuonya Twaha 'Kiduku' Kassim kwamba aache kumuwaza Mwakinyo kwani si levo yake kwa sasa.

Mwakinyo ametetea ubingwa wa Afrika (ABU) kwa kumchapa Julius Indongo wa Namibia kwa TKO raundi ya nne ya pambano lililokuwa la raundi 12 la uzani w super welter lililopigwa jijini Dar es Salaam.

Dakika ya kwanza ya raundi ya nne, Indongo alichapwa konde lililompa sawia kwenye shavu la kulia na kumtikisa, akaenda chini kana kwamba ameteleza na kunyanyuka haraka kisha kurudi kwenye kwenye kona yake ya bluu wakati refarii akimhesabia na yeye kucheka uku akimtazima usoni.

Wakati akihesabiwa, baadhi ya mashabiki ukumbini, walipinga na kudai halikuwa shambulio la refarii kumhesabia bondia huyo aliyekuwa akishangiliwa na mashabiki wachache kutoka ubalozi wa Namibia nchini.

Sekunde chache baadae, pambano liliendelea na Indongo kushambuliwa akiwa amebananishwa kwenye kona bila kujibu mashambulizi, hali iliyopelekea mashabiki wengi ukumbini kusimama na kumshangilia kwa nguvu Mwakinyo, kabla ya refarii kumuokoa.

Indongo aliegemea kamba za ulingo na kuwageukia mashabiki huku akitabasamu, kabla ya Mwakinyo kumfuata na kumkumbatia kwa ishara ya 'fair play' dakika chache kabla ya kuvikwa kwa mara nyingine taji la ubingwa wa Afrika (ABU) na mkuu wa mkoa wa Tanga, Adam Malima

Raundi ya kwanza hadi ya tatu, mabondia hao walishambuliana kwa kupokezana, huku Indongo akiwa wa kwanza kurusha ngumi na Mwakinyo alisubiri hadi dakika ya pili ya raundi ya kwanza kurusha ngumi kwa mpinzani wake mara baada ya refarii kuanzisha pambano hilo saa 5:59 usiku.

Indongo ndiye alikuwa wa kwanza kurusha ngumi ya kulia iliyotua tumboni kwa Mwakinyo, ambaye kwa dakika moja aliweka 'guard' usoni, na kujibu mashambulizi kwa kushtukiza uku konde lake la kushoto likitua kwenye shavu la kulia la Indongo na kumfanya apepesuke, lakini alitulia na kujibu mashambulizi kwa kurusha konde lilomrudisha nyuma Mwakinyo .

Dakika ya tatu ya raundi hiyo, konde la Mwakinyo lilitua kwenye shavu la kulia la Indongo na kumfanya apepesuke kama awali, alipotulia alimbananisha Mwakinyo kwenye kona na kumpiga ngumi kadhaa za tumbo, bondia huyo akiwa ameweka 'guard' usoni kabla ya kengere ya kulia.

Raundi ya pili, Mwakinyo alirudi vizuri na kumtandika ngumi kadhaa mpinzani wake ambaye alikwenda chini, lakini akawahi kukunja goti na refarii hakumhesabia, huku raundi hii, Mwakinyo akishambulia kwa kustukiza na wakati huo huo akiimalisha 'guard', mtindo alioingia nao hadi raundi ya tatu na aliporejea raundi ya nne alimaliza pambano kwa TKO.

Baada ya ushindi huo, Mwakinyo alisema hiyo ndiyo ilikuwa ndoto yake, aliomba apate matokeo hayo baada ya mpinzani wake kuonyesha dharau na kutamba yeye ni bondia wa kimataifa huku baadhi ya mashabiki wa Mwakinyo wakishangilia na kumtaja Kiduku ambaye kwa muda mrefu anatamani kucheza na Mwakinyo, lakini bondia huyo namba moja nchini anamuwekea ngumu.

Mashabiki hao walisema kwa ngumi anazopigana Mwakinyo sasa, Kiduku aanze kufuta wazo la kucheza naye kwani atakalishwa mapema tu.

Hata hivyo kocha wa Kiduku, Power Ilanda amesema tayari wamemuondoa bondia huyo kwenye mipango yao kwa kuwa hana nia ya pambano hilo na sasa Kiduku anapigania uzani tofauti na ule wa Mwakinyo, hata kwenye ubora Mwakinyo yuko juu kidunia.

"Mwakinyo ni levo nyingine, anacheza ngumi za akili, ana punchi zenye nguvu na anapokuwa uligoni anajitoa kufa au kupona, hapa nchini bado sijaona bondia wa kumpiga," alisema mmoja wa makocha wa ngumi aliyekuwa ukumbini hapo.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz