Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwakinyo amtupia dongo tena Twaha Kiduku "Bendera puto"

Kiduku Mwaki Mwakinyo amtupia dongo tena Twaha Kiduku "Bendera puto"

Mon, 31 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia Hassan Mwakinyo ameendelea kumpopoa hasimu wake, Twaha Kiduku kwa maneno ya kejeli baada ya bondia huyo kutoka Morogoro kupigwa katika pambano lake dhidi ya Asemahile Wellem wa nchini afrika Kusini.

Katika pambano hilo lililopigwa usiku wa juzi Julai, 29, 2023 katika ukumbi wa Malaika Beach Resort, Mwanza, Kiduku ambaye hujiita bendera chuma, mlingoti chuma, alipigwa na Wellem kwa pointi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mwakinyo ameandika; "Bendera puto, mlingoti sindano. Kuna mambo ni madogo lakini yakitokea yanaweza kukupa furaha ya mwaka mzima," amesema Mwakinyo.

Pambano hilo la raundi 12 lilikuwa la kuwania Ubingwa wa WBF Intercontinental (Ubingwa wa Mabara) katika uzito wa super middleweight limemfanya Bondia Asemahle kucheza pambano lake la 7 bila kupoteza wakati Kiduku mara ya mwisho kupoteza pambano ilikuwa Mei 20, 2021 dhidi ya Bek Nurmaganbet wa Kazakhstan.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live