Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwakinyo amdunda Mghana

Mqakinyo 82 Mwakinyo amdunda Mghana

Sun, 2 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Sakata la pambano la Bondia Hassan Mwakinyo na Patrick Allotey kutoka Ghana limemalizika rasmi baada ya wawili hao kuzichapa usiku wa kuamkia leo.

Mwakinyo ameshinda pambano hilo lilofanyika Dar es salaam kwa TKO baada ya Allotey kushindwa kuendelea na pambano raundi ya pili ilipomalizika akieleza kuwa ameumia bega na ndipo 'Champez' alipotangazwa mshindi.

Hata hivyo katika raundi hizo mbili Mwakinyo alionesha uchu wa kutaka ushindi akirusha makonde mazito kwa mpinzani wake.

Ushindi huo unamfanya bondia huyo kutetea mkanda wake wa ubingwa wa WBO.

Pambano hilo lilipaswa kupigwa usiku wa Mei 31, 2024 lakini ilishindikana kutokana na Mwakilishi kutoka WBO kutolipwa fedha zake kitendo ambacho Mwakinyo amenukuliwa akisema kinautia doa mchezo wa ngumi huku akitupa lawama kwa promota wa pambano hilo.

Kanuni zinaeleza kuwa Mwakinyo asingecheza mchezo huo angepokonywa mkanda huo hivyo bondia huyo alilazimika kuchipa usiku wa jana baada ya vikao vingi vya kujadili hatma ya pambano hilo kufanyika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live