Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwakinyo afunguka kuhusu kubaniwa na Media

Hassan Mwakinyo Jrrrr Mwakinyo afunguka kuhusu kubaniwa na Media

Tue, 4 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ameandika Bondia @hassanmwakinyojr

Guys naomba niombe radhi mashabiki wangu wote na niweke wazi kitu kimoja kulingana na sitofahamu iliyotokea juzi kwa mimi kutokucheza kwenye pambano langu lilo tarajiwa na wengi wenu, NAOMBA NIANDIKE KWA HERUFI KUBWA YA KWAMBA AZAM TV HAWANA CHUKI WALA BIFU YOYOTE NA MIMI kama inavyo tafsiriwa na wengi"

"Binafsi kilichotokea juzi wamejitahidi sana kupambana kisitokee nimeona jitihada zao kubwa sana zikifanyika kunusuru lile pambano kuanzia ngazi za juu mpaka chini ya uongozi, yani hata kulipokuwa na taarifa ya pambano kufutwa na uongozi wa chama cha ngumi ilikuwa ni Sawa kabisa kulingana walishaona kuna mapungufu mengi ambayo walijua yangetokea haya"

"Anyway kiufupi ipo haja sasa ya sisi wapiganaji kupewa fursa na kipaumbele cha kufanya kazi kupitia promoshen zetu hii itasaidia kuepeusha matatizo ya lazima yanayo węża kujitokeza kwa mapromoter wahuni waongo kama ilivyotokea"

"Na ni vile tu sasa nimekua nafikiri zaidi kabla ya kufanya kitu lakini kama nisingefanikiwa kupigana lile pambano jana kwa jitihada zangu binafsi basi huwenda sasa ningekuwa Oysterbay Police kwa jinai Mbaya kubwa ambayo pengine ingepumbazisha fikra na akili ya kila ambae angeskia kuhusu"

"Nawashukuru sana mashabiki zangu ambao hawakusita kufika na kuungana na mimi na wote ambao wamekua wakifuatilia wakati wote Mwenyezi Mungu atawalipa zaidi ya mapenzi yenu"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live