Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwakinyo, Tony Rashid Ulingoni Februari 25

Tony Mwaki Mwakinyo, Tony Rashid Ulingoni Februari 25

Fri, 11 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia namba moja Tanzania, Hassan Mwakinyo, anatarajia kurejea ulingoni Februari 25 mwaka huu, katika msimu wa pili wa pambano la 'MABINGWA WA ULINGO' litakalopigwa ukumbi wa ubungo Plaza, jijini Dar es salaam.

Ambapo siku hiyo kutakuwa na mapambano makuu mawili, moja Tony Rashid atarudiana na bondia kutoka Afrika kusini, Bongani Mahlangu, baada ya awali mwezi Septemba mwaka jana Tony kupoteza ubingwa wake wa ABU mbele ya bondia huyo.

Mwakinyo yeye anatarajiwa kucheza pambano lisilo la ubingwa, dhidi ya bondia namba nne kwa ubora nchini Venezuela, Ivan Matute, mwenye rekodi ya kucheza jumla ya mapambano 34 ya ngumi za kulipwa.

Bondia huyo, Katika mapambano 34 aliyocheza, ameshinda mapambano 30, 25 akishinda kwa KO na kupoteza mapambano manne, mawili akipigwa kwa KO.

Matute mwenye umri wa miaka 28, ni bondia mwenye nyota mbili, akishika nafasi ya 195 kati ya mabondia 1764 wa daraja la Super Welterweight duniani.

Bondia huyu, alianza kucheza ngumi za kulipwa mwezi Oktoba mwaka 2014, akishinda kwa TKO dhidi ya Noel Gomes.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live