Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwakinyo: Tanzania hatuna walimu wazuri wazuri

Hassan Mwakinyo Bondia Hassan Mwakinyo

Tue, 5 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Wiki iliyopita Bondia Seleman Kidunda kupata sare na Bondia kutoka Afrika ya kusini.

Bondia Hassan Mwakinyo alikuwa na haya ya kusema;

"Naomba nitoe elimu kidogo wasena zangu japo inaweza kukwaza wengine lakini sio lengo langu lengo ni kutoa elimu tu kwa maslah na faida ya watanzania wote. Okay.. Tanzania ina wapiganaji wazuri wenye sifa na viwango vikubwa lakini kwa bahati mbaya na isiyo rafiki kwetu tumekosa walimu wazuri wenye sifa sawa na uwezo wa wapiganaji wao hivyo kupelekea kushindwa kusogeza viwango vya wapiganaji wao na hii ni kwa sababu pia hatuna vyuo madhubuti vya ufundishaji wa ngumi kwa walimu wetu Kwenda kusoma eidha hawana uwezo wa kujilipia wao binfsi kusoma."

"Msicho kifaham ni kua mpiganaji yoyote wa Tanzania akiwa ulingoni asilimia 40% Ni akili yake binafsi na asilimia 60% Ni kutoka kwa kocha Wake inapofikia mahali kocha, akakosa cha kusema kwa taharuki uwanjani juu ya taaaluma ambayo anaifanya kwa mazoea na uwelewa tu na sio kua ana elimu nayo. Hivyo inampelekea bondia kukosa kabisa cha kufanya na hapo ndio madhaifu huonekana kua mengi uwanjani na mambo kuonekana kuharbiki"

"Ni kwa bahati sana kukuta nyuma ya bondia mzuri kuna walim wazuri wanao elewa cha kufanya badala yake. Kama kuna watu walio kua karbu ya kona ya bondia mgeni juzi waligundua kua yule bondia hafanyi kitu mpaka waseme walimu wake sisi hatuna ule mfumo mimi binafsi sijawah kuona lakini lile kwetu ni somo tunapaswa kujifunza lakini Pia hio haimaanishi kua sisi Ni dhaifu au hatufai kabisa.

"Lakini yanapotokea makosa tukosoe kidogo tusifie zaidi na mwisho wa safari ya maneno ya kashfa na vicheko vyote sisi Ni watanzania na ndio kwanza tumeanza kunyanyuka sasa kwenye mchezo wetu hivyo inatupasa kutia zaidi wachezaji wetu moyo sio kuwa vunja na tukiacha ushabiki preparation za kwetu na wenzetu Ni tofauti sana kuanzia *mental health, fight strategy* consistency of preparation.. how to beat your opponent.. na vyote hivyo sisi hatuna zaidi ya Rehema za Mungu na mtume wake"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live