Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwakinyo: Siwezi kupigana na bondia wa Tanzania

Mwakinyo Hassan 3 Siwezi kupigana na bondia wa Tanzania

Wed, 29 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia kinara wa Tanzania, Halfan Hythani Hamza 'Hassan Mwakinyo' amesema kuwa yeye hawezikupigana na mabondia wa Tanzania kwani kwa kufanya hivyo ni kama kujishusha kiwango ikizingatiwa yeye ameshapanda mpaka viwango vya dunia vya masumbwi.

Mwakinyo, 28, amewahi kushinda ubingwa wa Dunia UBO kwa kumchakaza Muingereza, Sam Eggington na kupanda mpaka kwenye top 10 ya ubora katika uzani wa super welter.

"Mimi kupigana na bondia wa Tanzania hilo kwangu haliwezekani hata niwekewe Trillion kumi.

"Kwanini nipigane na bondi wa Tanzania wakati wao wananiangalia mimi kama role model wao, wanatamani kuwa kama mimi sasa kwanini nijishushe niwe kama wao na wengi wanatamani kufika nilipofika?," Hassan Mwakinyo.

Baada ya kupita mwaka mmoja baada ya kupigwa na Liam Smith kwa TKO Echo Arena, Liverpool nchini Uingereza huku akidai kuwa kiatu chache kilikuwa kikimchoma, sasa atapanda tena ulingoni jijini dodoma mwezi Aprili na Kuseva Katembo kutoka Afrika Kusini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live