Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwakinyo: Simwogopi Twaha Kiduku, promota akifika bei tunazichapa

Mwakinyo Kiduku Ms Mwakinyo: Simwogopi Twaha Kiduku, promota akifika bei tunazichapa

Tue, 2 Jan 2024 Chanzo: Mwakinyo: Simwogopi Twaha Kiduku, promota akifika bei tunazichapa

Bondia Staa Hassan Mwakinyo amesema hamuogopi Bondlia mwenzake Staa Twaha Lubaha maarufu kama Twaha Kiduku na kwamba kama atatokea promota kwake ni jambo dogo kauli ambayo inaashiria yupo tayari kupigana nae.

Akiongea na Waandishi wa tabari leo Palm Village Jijini Dar es Salaam kuelekea pambano lake la Januari 27, 2024 Zanzibar, Mwakinyo amesema akiwa na umri wa miaka 18 alipigana na Bondia Maisha Samson na kumpiga licha ya Bondia huyo kuwa na mwili mkubwa hivyo hamuhofii Kiduku.

Akijibu swali la Mwandishi kuhusu kama anaweza kupigana na Kiduku, Mwakinyo amesema;

"Huyu mnayemuona hapa (kwenye picha kupitia simu yake) anaitwa Samson Maisha wa Mbeya, nilipigana nae nikiwa na miaka 18, ni Boxer ambaye lilipoandaliwa pambano Tanga, Mji mzima waliumwa matumbo kutokana na mwonekano wake anaoonekana nao hapa lakini nilipigana kiume na nilishinda hilo pambano kwa TKO raundi ya pili."

"Hii naiweka wazi kwa ambao wanafikiri yule Dada yao kule Morogoro wakafikiria kwamba labda nitakuwa nahofia Maboxer wenye miili mikubwa.

"Kinachonipa hamasa zaidi ni zile piko anazozipaka kwa sababu Marehemu Bi. Fatma Mama yangu alikuwa ni kungwi anawafundisha Mabibi Harusi, kwa hiyo nimezoea zaidi kuona piko nikiwa nyumbani.

"Kwa hiyo Mapromota wakitokea nao kama hili suala wana interest nalo basi InshaAllah tuendeleeni kuvuta uradi tumswalie sana Mtume nafikiri ni jambo dogo sana."

Mwakinyo anatarajiwa kupanda ulingoni tena January 27, 2024 kwenye ukumbi mpya uliopo ndani ya New Amaan Complex visiwani Zanzibar kupambana na Bondia wa Zimbabwe, Enock Msambuzi kwenye pambano litakalofahamika kama pambano la Mtata Mtatuzi.

Chanzo: Mwakinyo: Simwogopi Twaha Kiduku, promota akifika bei tunazichapa