Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwakinyo, Mnamibia ulingoni Septemba

Hassan Mwakinyo Bondia Mtanzania, Hassan Mwakinyo

Fri, 13 Aug 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Bondia Hassan Mwakinyo sasa atapanda ulingoni Septemba 3 kuzichapa dhidi ya Mnamibia, Julius Indongo huku rekodi zikionekana kumbeba Mtanzania huyo.

Pambano hilo ambalo awali lilikuwa lipigwe Julai kabla ya kufutwa litafanyika jijini Dar es Salaam kwenye Ukumbi wa Kilimanjaro uliopo kwenye Hoteli ya Ubungo Plaza.

Mwakinyo atapanda ulingoni akiwa amepanda ubora na kuwa bondia wa nyota nne anayekamata namba 37 ya dunia kwenye uzani wa super welter na mpinzani wake ni bondia wa 52 mwenye nyota tatu.

Promota wa pambano hilo, Amosi Martin (Amoma) alisema maandalizi yanakwenda vizuri ikiwamo mabondia kusaini mkataba.

Pambano hilo litakuwa la ubingwa wa African Boxing Union (ABU) la uzani wa super welter ambao Mwakinyo atakuwa akiutetea.

Uzoefu utakuwa ukimbeba zaidi Indongo kwenye pambano hilo la raundi 12 huku Mwakinyo akibebwa na rekodi.

Mnamibia huyo aliyewahi kuchapwa na bondia namba moja wa dunia, Terence Crawford atamkabili Mwakinyo akiwa amecheza mapambano 26 na kushinda 23 huku Mwakinyo akiwa amepigana mapambano 21 na kushinda 19.

Katika mapambano matano ya karibuni, Mwakinyo ameshinda yote na Indongo ameshinda mara tatu. Pambano hilo litasindikizwa na mengine sita likiwamo la ubingwa wa ABU la uzani wa bantam kati ya Mtanzania, Tony Rashid dhidi ya Bongani Mahlangu.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz