Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwakinyo, Mfilipino waanza tambo

84238 Mwakinyio+pic Mwakinyo, Mfilipino waanza tambo

Fri, 15 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Bondia Arnel Tinampay wa Philippines amemtaka Hassan Mwakinyo kujiandaa kwa kipigo kwa kuwa anafahamu ubora na udhaifu wake.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari Philippines vilimkariri bondia huyo akitamba kushinda pambano hilo litakalofanyika Novemba 29, Dar es Salaam.

Tinampay bondia namba moja nchini humo kwenye uzani wa super welter alisema anakuja nchini kuendeleza wimbi la ushindi.

Hata hivyo, Tinampay alisema Mwakinyo ni bondia bora Afrika kwenye uzani wa super welter akishika namba barani humo na 19 duniani.

“Natokea Philippines watu wa ngumi wanafahamu ubora wa mabondia wa huko, nakuja Tanzania, Mwakinyo ujiandae, nimemfuatilia najua ana ngumi nzito, lakini nitahakikisha nampiga KO,” alisema bondia huyo.

Wakati Tinampay akitamba, Mwakinyo amewatoa hofu Watanzania kuhusu pambano hilo na anafanya mazoezi ya kutosha.

“Mashabiki wangu wasishtushwe na tambo zake, hawezi kunipiga KO niko fiti nimejipanga kuweka rekodi ya kushinda kwa KO mbaya,” alitamba Mwakinyo.

Bondia huyo ambaye amepiga kambi kwenye milima ya Usambara, Lushoto alisema atamkabili Tinampay kwa nguvu na mkakati wake ni kushinda.

Tinampay atawasili Novemba 18 alfajiri na atafanya mazoezi ya wazi Dar es Salaam na Tanga kabla ya kupanda ulingoni kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Chanzo: mwananchi.co.tz