Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwakinyo, Mfilipino uso kwa uso Dar es Salaam leo

85111 Pic+ngumi Mwakinyo, Mfilipino uso kwa uso Dar es Salaam leo

Fri, 22 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Hatimaye mabondia Hassan Mwakinyo na Arnel Tinampay wa Philippines watakutana kwa mara ya kwanza leo Jumatano katika hoteli ya Serena kuanzia saa 5:00 asubuhi ikiwa ni siku tisa kabla ya kuzichapa Novemba 29.

Mabondia hao wamekuwa wakitambiana kila mmoja akijinasibu kushinda kwa matokeo yasiyokuwa na utata ya Knock Out (KO) watakutana kwa mara ya kwanza Leo jijini Dar es Salaam kuzungumzia pambano lao.

Mwakinyo na Tinampay wamekuwa na tambo za mara kwa mara tangu waliposaini mkataba wa kuzichapa pambano hilo la Novemba 29 litakalopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Tayari Tinampay amewasili Jumatatu ambapo ameweka kambi jijini Dar es Salaam, huku ile ya Mwakinyo ikiendelea Lushoto, Tanga.

Promota wa pambano, Jay Msangi amesema wamelazimka kuwakutanisha mabondia hao ili kuongeza hamasa ya ushindani baina yao.

"Watakutana katika hoteli ya Serena kuanzia saa 5:00 asubuhi, tumefanya hivi kutokana na tambo za pande zote mbili, kila mmoja amekuwa akijianasibu kumchakaza mpinzani wake kwa KO.

"Hivyo watakapokuatana laivu kutaongeza hamasa zaidi ya ushindani kuelekea kwenye zoezi la kupima uzito na afya tayari kwa pambano hilo," alisema Msangi.

Chanzo: mwananchi.co.tz