Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwakinyo: Mcongo hanitishi kwa lolote

Mwakinyo+pic Mwakinyo: Mcongo hanitishi kwa lolote

Tue, 11 Aug 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Imani MakongoroWAKATI homa ya kuwania ubingwa wa mabara wa WBF kati a Hassan Mwakinyo na Tshibangu Kayembe ikipanda, Mwakinyo amewatoa hofu mashabiki wake akisisitiza kuwa mpinzani wake raia wa DR Congo hamtishi kwa lolote.

Mabondia hao watazichapa Ijumaa ijayo pambano la raundi 12 la uzani wa super welter litakalopigwa kwenye ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

Mpinzani wa Mwakinyo anatarajiwa kuwasili nchini wakati wowote kuanzia sasa  tayari kwa zoezi la kupima uzito na afya litakalofanyika keshokutwa Alhamisi.

Mwakinyo anatarajiwa kuwasili Dar es Salaam kesho Jumatano akitokea Tanga ilipo kambi yake, ambayo anasisitiza kuwa ni kambi ya mafanikio.

"Mashabiki wangu wajiandae kupokea ubingwa, Mcongo hanitishi kwa lolote," amesema Mwakinyo.

"Ninachosubiri ni siku ya pambano ifike, mashabiki wangu wakae mkao wa kusherehekea ubingwa mapema, hata iweje Tshbangu hawezi kunipiga," amejinasibu Mwakinyo ambaye ana rekodi ya kucheza mapambano 18 na kushinda 16.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz