Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwakinyo, Liam Smith kupima uzito Liverpool

Mwakinyo Banner 1 1140x640 Mwakinyo, Liam Smith kupima uzito Liverpool

Fri, 2 Sep 2022 Chanzo: dar24.com

Bondia Hassan Mwakinyo na Mpinzani wake Liam Smith leo Ijumaa (Septemba 02) watapima uzito kuelekea Pambano lao litakalounguruma kesho Jumamosi (Septemba 03).

Pambano hilo la Raundi 12 litapigwa Uingereza katika ukumbi wa M&S Bank Arena ndani ya jiji la Liverpool nchini Uingereza kwenye pambano.

Mwakinyo atapanda ulingoni akizidiwa ubora (Rekodi na Uzoefu) na Mpinzani wake Smith, ila endapo Bondia huyo kutoka Tanzania atashinda, ataandika historia mpya kwenye rekodi ya Ndondi duniani.

Kwa mujibu wa mtandao wa ngumi za kulipwa wa dunia (Boxrec), Liam Smith amepigana mapambano 35 na kushinda 31, huku akipigwa mara tatu na kutoka sare mara moja tangu mwaka 2008.

Kwa upande wa Mwakinyo amepigana mapambano 22, ameshinda mara 20 na kupigwa mara mbili tangu 2015.

Chanzo: dar24.com