Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwakinyo: Bora kugawa chakula kilichoandaliwa kuliko kukimwaga

Mwakinyo Gloves .jpeg Mwakinyo: Bora kugawa chakula kilichoandaliwa kuliko kukimwaga

Thu, 28 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kupitia Insta Story ya bondia, Hassan Mwakinyo ameelezea mabadiliko ya mpinzani katika pambano la usiku wa Septemba 29, 2023 lililobatizwa jina 'The Return of Champ'.

Mpinzani mpya wa Mwakinyo (28) ni Julius Indongo (40), raia wa Namibia, bingwa wa zamani wa dunia kwa uzito wa chini atakaye pambana badala ya bondia namba moja wa Kenya Rayton Okwiri (37) katika pambano la Uzito wa kati la Kimataifa la Mabara (IBA).

"Napenda kuwataarifu mashabiki zangu yakuwa kumetokea mabadiliko kidogo juu ya kubadilishwa mpinzani," imenukuliwa sehemu ya andiko la Mwakinyo

Aidha, Mwakinyo amesema hajaridhishwa na mabadiliko hayo lakini amewaahidi kupambana ili kuwaridhisha mashabiki wake.

"Binafsi sijaridhishwa na mabadiliko haya lakini ni bora kugawa chakula kilichokwisha andaliwa kuliko kutupa. Natumai mashabiki zangu ni waungwana na kwa pamoja mtaelewa mabadiliko haya," amemaliza Mwakinyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live