Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwakinyo: BMT simamieni haki za Mnamibia, Promota hamtambui

Hassan Mwakinyo Jrrrr Bondia Hassan Mwakinyo

Fri, 29 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo amethibitisha kuwa hakutakuwa na pambano lake dhidi ya Bondia kutoka Namibia, Julius Munyelele Indongo na kusitisha biashara ya ununuzi wa tiketi kwa ajili ya pambano lake hilo.

Aidha Mwakinyo ametoa ombi kwa Baraza la michezo Tanzania (BMT) kusimamia haki za Bondia Munyelele ambaye tayari yupo Nchini kwa ajili ya pambano hilo kwa mujibu wa sheria.

“Fight has been cancel baada ya mazungumzo kuto fika atamu na sasa ni rasmi hakutakua na pigano langu hakuna tena biashara ya kununua ticket ...

“Ombi kwa wizara ya michezo na BMT naomba wasimamie haki za bondia Julius Indongo amefika kwa ajili ya pambano na sheria ni kama pambano limevunjika kwa bondia mmoja inabidi mgeni alipwe haki zake kwakua yeye amefika.

“Naomba simamieni promoter amemkana anasema hamjui na haya mambo hayana mwenyewe na sisi huwa tunasifiri kwenda nchi za watu yanaweza tukuta pia i hope litafanyiwa kazi.!! Next time!! Wanasema kufa kwa Imamu sio mwisho wa swala...” ameandika Mwakinyo kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live