Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mukadi amchimba mkwara Seleman Kidunda

Mukami.png Mukadi amchimba mkwara Seleman Kidunda

Tue, 13 Jun 2023 Chanzo: Dar24

Bondia Erick Mukadi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, amesema anajiandaa vizuri kwa ajili ya pambano lake la Juni 30 dhidi ya Mtanzania Seman Kidunda na anakuja Tanzania kufuata ushindi kwa kumpiga mpinzani wake.

Mukadi ametoa kauli hiyo kuelekea katika pambano hilo lililoandaliwa na Kampuni ya PAF Promotion Company Limited huku likipewajina la ‘Hata usipolala Patakucha tu’ ambapo pia Mfaume Mfaume atapanda uliongoni dhidi ya Nkululeko Mhlongo wa Afrika Kusini.

Mukadi amesema anakuja Tanzania kwa kazi ya kuhakikisha anampiga vibaya Seleman Kidunda kutokana na maandalizi makubwa ambayo anaendelea kufanya.

“Nipo sawa naendelea na maandalizi yangu kwa ajili ya pambano langu na Kidunda, ninachotaka kumwambia kuwa nakuja Tanzania kumpiga Kidunda, tena nitampiga vibaya sana na kumfundisha ngumi,” amesema Mukadi.

Amesema Tanzania ikae tayari kwa sababu anakuja kufanya kitu kibaya kwa bondia wake na anafanya maandalizi makali ya kutoa kipigo na kutoa onyo kwa mabondia wengine wa Tanzania.

Siku hiyo ya Juni 30 kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi ambapo bondia Fadhili Majiha ‘Stopper’ atapanda ulingoni kupigana na Jamal Kunoga, Saleh Kasim atapigana na Said Bwanga na Deo Samweli atapigana na Adam Ngange.

Mengine Mapambano Pius Mpenda atapanda ulingoni dhidi ya Simon Tichecha wa Malawi wakati Rama John Cena akitarajia kupigana na Yona Segu, Omary Maulid atapanda ulingoni kupigana na Shaban Kibiriti, Boniface Seguda atapigana na Hamza Mahamoudu wakati Herry Rashid akitarajia kupigana na Hussein Pendeza.

Chanzo: Dar24