Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtanzania kuanza na mwenyeji ndondi za dunia

Boxing Pic Ndondi Mtanzania kuanza na mwenyeji ndondi za dunia

Wed, 15 Mar 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Beatrice Nyambega atafungua dimba kwa mabondia wa Tanzania keshokutwa Ijumaa kwenye mashindano ya ngumi ya dunia kwa wanawake yatakayofunguliwa kesho nchini India.

Beatrice atacheza na mwenyeji, Jasmine Jaismine kwenye uzani wa light kilogramu 60 kuanzia saa 9.30 alasiri ya Tanzania akiwa kona ya bluu.

Mtanzania mwingine, Rahma Maganga atapanda ulingoni Jumamosi dhidi ya Mkenya, Kwenye uzani wa Minimum kilogramu 48.

Rahma atacheza na Christine Ongare bondia aliyewahi kuzichapa naye Januari mwaka huu kwenye mashindano ya klabu bingwa Afrika Mashariki.

Mtanzania huyo alichapwa kwa pointi za majaji 3-2 na kwenye mashindano ya dunia anasema amedhamiria kulipa kisasi.

Chanzo: Mwanaspoti