Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msukuma kuzichapa na Makamba?

Makamba Gs Msukuma Msukuma na Makamba

Tue, 28 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuelekea pambano la Bondia Hassan Mwakinyo dhidi ya Kuvesa Katembo kutoka Afrika Kusini lenye lengo la kukusanya pesa za kununulia taulo za kike baadhi ya waheshimiwa wabunge wanatarajiwa kushiriki kwa kuingia Ulingoni siku hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari promota wa mchezo huo ambaye pia ni Mbunge, Sophia Mwakagenda amesema amewashawishi viongozi hao kumuunga mkono.

”Pambano la kwanza kwa wabunge kwa dakika tatu tatu, Msukumu (Joseph Kasheku) yeye anataka kucheza na January Makamba, lakini pia Babu Tale atacheza na Elibariki Kingu, Salome Makamba yeye atapambana na Neema Lugangira,” amesema Sophia Mwakagenda.

Mgeni rasmi katika mapambano hayo anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live