Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkongwe wa miaka 86 aweka rekodi ya kunyanyua vitu vizito

Mkongwe Wa Miaka 86 Aweka Rekodi Ya Kunyanyua Vitu Vizito Mkongwe wa miaka 86 aweka rekodi ya kunyanyua vitu vizito

Thu, 30 Mar 2023 Chanzo: Bbc

Mzee wa miaka 86 amevunja rekodi za dunia na kitaifa katika shindano lake la mwisho la kunyanyua vitu vyenye uzani mkubwa.

Brian Winslow alinyanyua kilo 75 katika jaribio lake la kwanza katika mashindano ya Jumuiya ya Kuinua vitu vizito Uingereza (BDFPA) yaliyofanyika Machi 18 2023.

Brian Winslow kutoka Derbyshire aliboresha rekodi ya kwanza kwa kuinua kilo 77 katika jaribio lake.

Bw Winslow sasa anashikilia Rekodi za Uingereza na Dunia katika kitengo cha kilo 60 kwa washindani wa kiume wenye umri wa miaka 85 hadi 89, kulingana na BDFPA.

Bw Winslow, ambaye alianza kunyanyua vitu vizito akiwa kijana alipokuwa akifanya kazi kama mhudumu kusini mwa Devon, alisema, "Nimefurahia."

Na kuongeza kuwa "Siku zote ni vizuri kupata rekodi moja au mbili. Nilikuwa nimechoka moja kwa moja lakini sawa."

"Kunyanyua uzani ni sehemu kubwa ya maisha yangu, pamoja na watoto wangu na wajukuu. Nitaendelea kwa muda kadiri mwili utakavyoniruhusu,” anasema.

Chanzo: Bbc