Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mike Tyson ampa jeuri Ngannou

Francis Ngannou Mike Tyson ampa jeuri Ngannou

Thu, 12 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Wapenzi wa masumbwi duniani wanahesabu siku tu kabla ya kushuhudia pambano kali la wababe wa kwenye ngumi na zile mchanganyiko (boxing, mixed) Tyson Fury na Francis Ngannou, ambao watapanda ulingoni kuzichapa Oktoba 28.

Pambano hilo la kwanza kwa Ngannou kupanda ulingo wa kawaida wa ngumi tofauti na aliozoea wa vizimba (octagon) na huku hakuna mateke wala kuangushana zaidi ya kuchapana makonde mazito ili kumwangusha mpinzani.

Saudi Arabia ndiko kutakapopigwa pambano hilo la uzito wa juu (heavyweight) lisilo na mkanda na gwiji wa masumbwi duniani, Mike ‘Iron’ Tyson amemtabiria ushindi bondia Ngannou ambaye pia ndiye anayemnoa kwa kumpa maujanja ya ngumi za kawaida.

Tyson amemweleza Ngannou kama bondia bora sana na amegundua hilo wakati anamnoa kujiandaa na pambano hilo.

Mike ametoa tahadhari ya watu kutoamini kitakachotokea endapo ngumi yoyote ya Ngannou ikampata Fury basi pambano litaishia hapo hapo kwa knockout ‘KO’.

Chanzo: Mwanaspoti