Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mhh! Ngumi za AJ muulize Ngannou

E242e6a0 Ddad 11ee Bfdf 0620afdaa448.jpeg Mhh! Ngumi za AJ muulize Ngannou

Sat, 9 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Bondia mwenye ngumi zito na zinazouma, Anthony Joshua amemkalisha kitako Francis Ngannou mara mbili kabla ya kumzima kabisa mara ta tatu na kuweka sawa njia yake ya kwenda kupambania ubingwa wa dunia wa uzito wa juu.

Bondia Ngannou, ambaye aliwahi kupigana na Tyson Fury kwa raundi 10 katika pambano lake la kwanza la masumbwi, Oktoba mwaka jana na alimwangusha WBC Gypsy King- hakufua dafu kabisa mbele ya Joshua katika pambano lao lililofanyika huko Riyadh, Saudi Arabia katika usiku wa kuamkia jana Jumamosi.

AJ alirusha ngumi kali sana na kumwangusha mpinzani wake kwenye raundi ya kwanza tu, kabla ya kumwangusha tena mapema raundi ya pili, kabla ya ile ya tatu, ambayo ilimfanya staa huyo wa zamani wa UFC kushindwa kuendelea na pambano baada ya kupigwa ngumi ya kumaliza pambano ambayo ilimwaacha bondia Ngannou wa Cameroon kuhitaji msaada wa kitabibu na alilazimika kuwekewa oksijeni.

Joshua alisema: “Ilivyo ndivyo ilivyo. Narejea kwenye mbio za ubingwa kama ambavyo inapaswa kuwa. Nilipoona pambano lake la Tyson Fury, niliona huyu jamaa anajua kupigana, nikamhitaji. Nilitaka kumkaribisha rasmi kwenye masumbwi. Sisemi asiendelee, anaweza kuja tena.”

Pambano lilivyoanza, Ngannou alirusha ngumi ya kushoto na kuonekana kama ingempa shida hivi AJ, kabla ya Mwingereza huyo kucharuka na kurusha makonde yaliyomweka chini mpinzani wake na kuanza kuhesabiwa na refa, nusura ashindwe kunyanyuka.

Ngannou aliangishwa tena kwenye raundi ya pili baada ya kupigwa ngumu ya kulia na kushoto, akahesabiwa tena, akanyanyuka fasta.

Baada ya mwamuzi kusema pambano liendelee, AJ alirusha ngumi iliyolegeza miguu ya Ngannou na kupiga magoti na baada ya hapo, bondia huyo wa Cameroon alionekana kuhitaji msaada wa kitabibu.

Sasa AJ anasubiri kuona kama atazipiga na Fury au Oleksandr Usyk - mtu ambaye alimpoka mikanda yake ya WBA, IBF na WBO ya ubingwa wa dunia kwa pointi.

Chanzo: Mwanaspoti