Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfaume kuwania mkanda wa WBF Afrika leo

MFAUME.jpeg Mfaume Mfaume anapanda ulingoni kwa mara ya kwanza baada ya miaka 2

Fri, 1 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia mtanzania Mfaume Mfaume atapanda ulingoni leo kwa mara ya kwanza baada ya miaka miwili kuwania ubingwa wa WBF Afrika uzito wa Welterwight dhidi ya Bondia kutoka Misri Abdulmonem Said. Pambano litakalofanyika ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es salaam kuanzia majira ya Saa 12 jioni.

Mfaume Mfaume amesema amejiandaa vizuri kuelekea Pambano hili na amewaahidi watanzania kupata ushindi hapo kesho kutoka na maandalizi mazuri aliyoyafanya.

“Nimepata maandalizi ya muda mrefu kwa hiyo watanzania watarajie kuona ngumi Biriani kwa uwezo wa Mungu watanzania watafurahi, kwa sababu ushindi wa Mfaume Mfaume ni ushindi wa Tanzania” Ameseme Mfaume

Kabla ya pambano hili yatafanyika mapambano mengine saba ya utangulizi ambapo Mwana dada Stumai Muki atacheza dhidi ya Chimwemwe Banda wa Malawi, Laurent Segu ataminyana na Thomas Mahaule, Pius Mpenda atazichana na George Dimoso, Issa Nampepeche dhidi ya Juma Choki, Oscar Richard anacheza na Bongani Makovora kutoka Zimbabwe, Hamisi Maya atanyukana na Murdochee Katembo wa Congo na Ibrahim Class atazichapa na Peter Pambeni wa Zimbabwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live