Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfaume amchakaza kwa Ko bondia kutoka Misri

WhatsApp Image 2022 07 02 At 12.jpeg Mfaume amchakaza kwa Ko bondia kutoka Misri

Sat, 2 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia wa Ngumi za kulipwa nchini Mfaume Mfaume ameshinda mkanda wa ubingwa wa Afrika (WBF) baada ya kushinda KO raundi ya pili dhidi ya mpinzani wake kutoka Misri Abdulmonen Said katika pambano la "Return of Naccoz King"

Aidha, bingwa huyo amesema alijiandaa vizuri aliweka kambi miezi mitatu Mkoani Morogoro Kwa ajili ya kupambania mkanda huo na kuiletea ushindi nchi ya Tanzania.

Hata hivyo Mfaume amesema ana tambua uwezo wa mpinzani wake kwani Kwa nchi ya Misri ni Bondia mzuri na ameshacheza mapambano 22 na yote amefanya vizuri huku pambano Moja akitoa sare na mpinzani wake.

Pia amesema ushindi huo ni Kwa Mashabiki zake na watanzania wote Kwa ujumla wanaopenda mchezo wa Masumbwi.

"Huu ubingwa ni watanzania wote nimeweza kubakisha mkanda nyumbani nashukuru Kwa wote waliohakikisha mkanda huu unakuwa wa watanzania".

Chanzo: www.tanzaniaweb.live