Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfaume: Sina bifu na Mwakinyo ila...

Mwakinyo 1 Pic Bondia Mtanzania, Hassan Mwakinyo (kushoto) akiwa ulingoni

Thu, 3 Mar 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Baada ya mashabiki wa mabondia Mfaume Mfaume na Hassan Mwakinyo kutupiana vijembe kwenye mitandao ya kijamii chanzo kikidaiwa ni bifu kati ya mabondia hao wanaofanya vizuri nchini, Mfaume amefunguka kila kitu kuhusu mgogoro huo akisisitiza hana bifu na Mwakinyo.

Mfaume bondia namba moja nchini kwenye uzani wa middle alisema sintofahamu hiyo ilianza baada ya Mwakinyo kutaka mtu wa kufanya naye mazoezi akiwa Dar es Salaam.

“Aliomba mtu wa kufanya naye sparing ‘mazoezi ya kupigana ana kwa ana’ shabiki wake mmoja akanitaja mimi, sikuwa na hiyana, nikakubali kufanya naye sparing ndipo yakaibuka maneno, lakini mimi sio mtu wa bifu.”

“Binafsi nilitaka sparing ifanyike kwenye ulingo ambao kambi yetu ya Naccoz ingegharimia kila kitu, wao wakakataa na kutaka sparing ya kwenye sakafu, nikawambia hiyo siyo sparing, ngumi gani zinapigwa kwenye sakafu?

“Hivyo sparing ile haikufanyika, ndipo yakaibuka maneno, lakini mimi sio mtu wa bifu na sina bifu na mtu ndiyo sababu nimekuwa kimya muda wote hata baada ya majibizano kuibuka kwenye mitandao ya kijamii,” alisema nahodha huyo wa kambi ya ngumi ya Naccoz.

Kuhusu kambi hiyo kumwongeza Juma Ngedere ambaye anatajwa kuongeza nguvu kuwanoa mabondia wa kambi hiyo, Mfaume alisema Ngedere ameomba kujiunga Naccoz kama wanavyojiunga wanachama wengine na si kuwa kocha.

“Naccoz ina watu na inapendwa hivyo Ngedere ameomba kujiunga nayo kama ilivyo kwa wanachama wengine na Naccoz haimkatai mtu, kikubwa ni aendane na falsafa ya kambi tu,” alisema.

Naccoz yenye maskani yake Mabibo jijini Dar es Salaam ni miongoni mwa kambi za ngumi maarufu nchini inayonolewa na Kocha Ramadhani ‘Jah’ Uhadi.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz