Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfaume Mfaume atoka hospitali

MFAUME.jpeg Bondia Mfaume Mfaume

Fri, 21 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Mfaume Mfaume ameruhusiwa kutoka hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dar ss Salaam Amana, baada ya kupata ajali ya bodaboda maeneo ya Tabata jijini humo.

Mfaume anayetoka gym ya Naccoz anayesimamiwa na Paf Promotion, amepata ajali hiyo jana usiku na kukimbizwa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Amana kwa matibabu zaidi akiwa na shabiki yake Cheduo anayetajwa kuvunjika mkono.

Akizungumza nasi, Mkurugenzi wa Paf Promotion, inayomsimamia bondia huyo, Fadhili Maogola amesema Mfaume amepata ajali hiyo jana saa mbili usiku alipokuwa anatoka kwenye kikao cha kazi katika eneo la Buguruni.

Kikao ambacho kilikuwa na viongozi wa menejimenti inayomsimamia kwenye kazi akiwa na shabiki wake Peter Mubarak ‘Cheduo ambaye alikuwa dereva wa pikipiki waliopata nayo ajali.

“Hali ya majeruhi hao inaendelea vizuri, Mfaume ametolewa hospital leo baada ya kupata matibabu ya majeraha aliyoyapata katika ajali hiyo, ameruhusiwa na yupo nyumbani,” amesema Mkurugenzi huyo.

Amewashusha presha ya mashabiki wa Mfaume na kuweka wazi kuwa bondia huyo hajapata majeraha makubwa wala hajavunjika zaidi ya kupata majeraha madogo madogo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live