Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchanjo amtambia Swalehe

113ce83b1d5bb5192d74407af62d92c2 Mchanjo amtambia Swalehe

Fri, 12 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

BONDIA, Haidari Mchanjo amesema baada ya kukimbiwa na mpinzani wake wa awali Loren Japhet, sasa yupo tayari kupigana na Mukhsin Swalehe kwenye pambano la usiku wa kisasi litakalofanyika Februari 27, Next Door Arena, Dar es Salaam katika pambano la raundi nane uzito wa kilogramu 57.

Akizungumza wakati akifanya mazoezi Ulongoni gym, Gongo la Mboto, Dar es Salaam jana, Mchanjo alisema kisasi alichotaka kumpiga Loren Japhet atakihamishia kwa Mukhsin kwani kwani atamnyoa ndevu zote ulingoni.

“Wewe Mukhsin au Alkasusu umedandia treni kwa mbele, tarehe 27 nitakupa kipigo cha mbwa mwizi na hizo ndevu zako nitazinyoa ulingoni kwani siyo saizi yangu,” alijigamba.

Mapambano mengine siku hiyo yatakuwa kati ya Fransic Miyeyusho na Habibu Pengo katika pambano la raundi nane uzani wa kilogramu 61, Mfaume Mfaumena Koba Donati pambano la raundi nane uzani wa kilogramu 69.

Naye Waziri Rosta atamvaa Mwinyi Mzengela raundi sita uzito wa kilogramu 63 na Baina Mazola atazichapa na Ismail Galiatano raundi nane uzito wa kilogramu 58.

George Bonabucha atajiuliza kwa Hashim Zuberi raundi sita uzito wa kilogramu 52, Beka Ustaadh dhidi ya Emmanuel Mwakyembe raundi nane uzito wa kilograamu 52 na Lukman Ramadhani atamaliza ubishi na Mohamed Mpombo pambano la raundi nane uzito wa kilogramu 52.

Chanzo: habarileo.co.tz