Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbelwa, Class watajwa orodha ya miamba 18 ya ndondi nchini

Bondia+pic Mbelwa, Class watajwa orodha ya miamba 18 ya ndondi nchini

Fri, 30 Apr 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Mabondia Said Mbelwa na Ibrahim Class ni miongoni mwa waliotajwa katika orodha ya mabondia 18 bora kwenye kila uzani nchini.

Katika orodha hiyo inayotolewa na mtandao wa ngumi za kulipwa wa dunia (Boxrec), mabondia hao wametajwa kuwa ni namba moja kwenye uzani wanaopigania.

Mbelwa bondia mwenye rekodi ya kucheza pambano la kwanza la ngumi za kulipwa nchini Afghanstan ametajwa kuwa bondia namba moja kwenye uzani wa juu mwepesi (light heavy).

Class bondia bingwa wa zamani wa GBC ametajwa kuwa kinara kwenye uzani wa super feather.

Katika orodha hiyo, bondia namba moja nchini kwenye kila uzani (pound for pound), Hassan Mwakinyo ndiye kinara pia kwenye uzani wake wa super welter.

Mabondia wengine waliokamata namba moja nchini ni Omari Shirika aliyetajwa kuwa kinara wa uzani wa juu (heavy).

Shirika amemuondoa kwenye ramani ya ndondi, bondia aliyekuwa akishikiria rekodi hiyo kwa muda mrefu, Alphonce Mchumiatumbo.

Mchumiatumbo ambaye katika ubora hivi sasa anaonekana hayupo 'active' ingawa hivi karibuni alichapwa kwa Knock Out (KO) na Jongo Jongo, pambano ambalo halijaingizwa kwenye rekodi.

Boxrec inaonyesha mara ya mwisho, Mchumiatumbo alichapwa kwa Technical Knock Out (TKO) nchini Russia Oktoba 5, 2019 na Arslan Iallyev.

Jongo ametajwa kuwa kinara kwenye uzani wa cruiser huku Twaha 'Kiduku' Kassim akiongoza kwenye uzani wa supper middle.

Wengine vinara nchini na uzani wanaopigania kwenye mabano ni Meshack Mwankemwa (middle), Idi Piarali (welter), Adam Kipenga (super light) na Salim Mtango amekuwa kinara kwenye uzani wa light.

Katika uzani wa feather, Muksini Swalehe (Mastiki the Don) ndiye kinara wakati Tony Rashid akiwa nyota kwenye uzani wa super bantam.

Charles Tondo (bantam), Innocent Evarist (super fly), Mustafa K Mkupasi    (fly),Muhsin Kizota (light fly) na Selemani Bangaiza anayepigania uzani wa Minimum ndiye amehitimisha orodha ya nyota 18 wa ndondi nchini.

Japhet Kaseba, Mfaume Mfaume na Mchumiatumbo ni miongoni mwa waliowahi kukalia usukani kwenye uzani wanaopigania, ingawa sasa wameporomoka.

Kaimu rais wa Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBRC), Agapeter 'Mnazareth' Basil alisema viwango hivyo vinatolewa kulingana na aina ya mapambano bondia aliyopigana.

"Ukicheza na bondia mkali zaidi yako ndivyo unapanda kwa haraka kama ukishinda," amesema.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz