Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbabe ataka kumchapa Kiduku kavukavu

Dullah+mbabe+kiduku+pic Mbabe ataka kumchapa Kiduku kavukavu

Thu, 27 Aug 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Imani MakongoroMashabiki wamelazimika kuingilia kati ili kumuamulia bondia Abdallah Pazi 'Dullah Mbabe' aliyetaka kuzichapa kavukavu na Twaha Kiduku wakati wa kupima uzito leo Agosti 27, 2020.

Mabondia hao ambao watazichapa kesho Ijumaa kuwania ubingwa wa Taifa katika uzani wa super middle wamepima uzito na afya kwenye Uwanja wa Kinesi, tayari kwa pambano hilo la raundi 12 la kuwania ubingwa wa Taifa kesho Ijumaa Agosti 28 kwenye uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Baada ya kupima uzito, Mbabe alipewa nafasi ya kuzungumza, lakini kabla ya kuongea chochote alimsukuma Kiduku ambaye hakujibu mashambulizi.

Hata hivyo Mbabe kabla hajafanya chochote kwa Kiduku, baadhi ya mashabiki walimshikiria huku akionekana kufoka na kumkebehi Kiduku ambaye muda wote alikuwa akitabasamu bila kujibu.

Tambo zatawala wakipima uzito

Wakati Twaha Kiduku akimueleza Dullah Mbabe kuwa hajui ngumi zaidi ya ubabe, bondia huyo amejibu mapigo akimwambia kuwa ajiandae kupokea kipigo cha kihistoria.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz