Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maugo amtangazia kiama mpinzani

Maugo Pic Maugo amtangazia Kiama mpinzani

Wed, 8 Jun 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Baada ya kuwa nje ya ulingo karibu miaka miwili, Mada Maugo ametangaza kurudi upya kwenye masumbwi huku akimtangazia kiama, Said Mbelwa watakayezichapa Julai 23.

Maugo atapanda ulingoni akizidiwa uzoefu na Mbelwa ambaye amesema hilo kwake sio tatizo na bondia huyo mwenye rekodi ya kucheza mapambao mengi nchini ndiyo atakuwa 'ngazi' yake ya kurudi kwenye masumbwi baada ya kufutwa kwenye renki.

"Nilikuwa sitaki kupigana naye muda mrefu na hata ngumi nilisimama tangu 2020, lakini kila mara alikuwa akienda kwenye mapambano yake ya 'ndondo' anasema namkimbia kwa kuwa namuogopa.

"Sikutaka kabisa kucheza naye sababu nilimuona kama mzee wangu, ana umri mkubwa kunizidi, nikawa naona nikicheza naye na kumpiga ni sawa na nimempiga mzee wangu, nilimuonea huruma, lakini maneno yalipozidi nikaona atanizoea, nikasaini kupigana naye, safari hii amekanyaga moto," alijinasibu bondia huyo.

Hata hivyo Mbelwa amesisitiza atapanda ulingoni si kushindana na Maugo bali kupigana naye japo anamuona si bondia wa levo ya kumtisha na bingwa atajulikana baada ya raundi zote kumalizika.

"Kwa mikiki ya ngumi niliyopitia, Maugo ni bondia wa kawaida kwangu, japo kwa Tanzania yuko kwenye levo za juu, lakini haingii kwa wale niliowahi kupigana nao kimataifa, namwambia tu kwamba nitakwenda kupigana naye siku hiyo na si kushindana naye,"amesema.

Pambano hilo la Chanika dabi ambalo litapigwa kwenye hoteli ya Butiama, limepangwa kuwa la raundi nane la uzani wa light heavy huku mabondia hao mmoja akishusha uzito na mwingine akipanda ili kuwa sawa.

Maugo ameshuka kutoka uzani wa cruiser na Mbelwa amepanda kutoka kwenye uzani wa super middle ambako ni bondia wa tano kati ya 35 wa uzani huo nchini, mara ya mwisho alipigwa kwa pointi nchini Russia na Artur Ter Israelyan, Mei 27 mwaka huu.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz