Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maugo: Kwa Mbelwa sitaki tena kesi

Mada Maugo Nakos.jpeg Bondia Mada Maugo

Sun, 24 Jul 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Baada ya kuibuka mshindi kwa pointi usiku wa kuamkia jana, bondia Mada Maugo amesema hana mpango wa kucheza pambano la marudiano na Said Mbelwa.

Mabondia hao walizichapa kwenye pambano la dabi ya Chanika, la raundi nane la uzani wa juu mwepesi lililokwisha kwa Maugo kutwaa ushindi wa pointi.

"Nimempiga hadi mkono ukaniuma, lakini yumo tu, alikomaa hadi mwisho, yule jamaa ni kiboko," ametamba Maugo baada ya kutangazwa mshindi.

Amesema kwa namna alivyompiga mpinzani wake, ikitokea akaomba pambano la marudiano huenda akampa kesi, hivyo hatakubali kurudiana na bondia huyo.

"Niliambiwa namuogopa na kumkimbia, lakini nimezungumza kwa vitendo ulingoni baada ya kumpiga kipigo 'hevi' mbele ya mashabiki wake muhimu.

"Nilimwambia hawezi kunipiga kwa vyovyote vile na ndicho kimetokea, ila pamoja na kushinda kwa kumpa kipigo cha nguvu, lakini nimemkukubali, Mbelwa anavumilia ngumi, nimempiga hadi miko yangu inauma, lakini alikomaa na kumaliza raundi zote nane, kongole kwake.

"Lakini kama nilivyosema, sitokubali kurudiana naye, maana kipigo nilichompa namuonea huruma nikiruhusu pambano la marudiano litanipa kesi," alitamba bondia huyo wa uzani wa juu mwepesi.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz