Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matumla: Dulla Mbabe atamchakaza Katompa

Image 610 1140x640.png Matumla: Dulla Mbabe atamchakaza Katompa

Sat, 17 Jun 2023 Chanzo: Dar24

Bingwa wa zamani wa Dunia wa Mkanda wa WBU, Rashid Matumla amesema kwa mwenendo mzuri wa Bondia Abdallah Pazi ‘Dulla Mbabe’ unaonesha amebadilika na anaweza kufanya vizuri katika pambano lake lijalo.

Dulla Mbabe anatarajiwa kupanda ulingoni Julai 15, mwaka huu katika usiku wa kisasi dhidi ya bondia kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Eric Katompa pambano litakalochezwa kwenye Uwanja wa Kinesi.

Matumla amesema amemfuatilia Dulla Mbabe kwenye mapambano ya hivi karibuni na ameona amebadilika kiasi kwamba anaweza kulipa kisasi kwa mpinzani wake Katompa aliyewahi kumpiga mwaka juzi.

“Dulla kabadilika, nimeshamwona kwenye mechi fulani, anachonifurahisha anajiamini, kabadilisha mchezo wake atafanya vizuri,” amesema Matumla. Bingwa wa zamani wa Dunia wa Mkanda wa WBU, Rashid Matumla

Kwa upande wake Dulla alisema kwa mazoezi aliyofanya chini ya kocha mkongwe, Habibu Kinyogoli anaamini anaweza kushinda na kumtaka ajiandae kulicheza sebene la kizaramo.

Naye Mratibu wa pambano hilo, Seleman Semunyu amehimiza wadau mbalimbali wa mchezo huo wajitokeze kusapoti pambano hilo na kuwaunga mkono vijana wanaotegemea kazi hiyo kuendesha maisha yao.

Semunyu amesema kabla ya pambano hilo, watafanya shindano la kutafuta bingwa wa kitaa lenye lengo la kuibua vipaji vya ngumi Temeke, Kinondoni na Ubungo na wale watakaofanya vizuri watachaguliwa kusindikiza pambano la Dulla.

Chanzo: Dar24