Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mandonga kuzichapa tena na Wanyonyi

Mandonga Wanyonyi .jpeg Mandonga na Wanyonyi

Mon, 22 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya pambano la kufana la kwanza miezi michache iliyopita, sasa wanasema usubiri kwa hamu pambano la marudiano la uzito wa juu litalowakutanisha tena “Mandonga na Wanyonyi 2” ambalo litatikisa Kituo cha maonyesho cha Sarit Julai 22, mwaka huu kwa mujibu gazeti la Daily Nation.

Mwanamasubwi wa Tanzania, Karim maarufu kama Mandonga “Mtu Kazi”, ambaye ni bingwa wa Pugilistic Syndicate of Tanzania (PST), na Daniel Wanyonyi, bingwa wa zamani wa taji la African Boxing Union (ABU) Kenya, Ijumaa walitupiana maneno ya kukosoana kama ilivyo kawaida kwa wapinzani kabla ya mechi yao ya marudiano iliyokuwa ikitarajiwa kufanyika jijini Nairobi.

Afisa mkuu mtendaji wa kusimamia mashindano ya Ultra Fight Series Maurice Odera alifichua Ijumaa kuwa Mandonga na Wanyonyi wametia saini mkataba wa kukutana tena kwenye mchuano wa “Marudio au Kulipiza kisasi”

Mandonga alimshinda Wanyonyi walipokutana kwa mara ya kwanza Januari 14, mwaka huu nchini Kenya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live