Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mandonga azawadiwa ndinga

Sfs Mandonga (2) Mandonga azawadiwa ndinga

Wed, 18 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia Mtanzania Karim Mandonga amekabidhiwa gari aliyoahidiwa endapo angeshinda pambano lake nchini Kenya.

Bondia huyo mwenye mbwembwe nyingi ndani na nje ya Ulingo, amepewa zawadi ya gari hilo aina ya Nadia na Mfanyabiashara Dick Sound bila mashariti yoyote, ikiwa ni sehemu ya kutimiza ahadi aliyokuwa ameahidiwa endapo angeshinda pambano la mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Bondia wa Kenya Daniel Wanyonyi.

Tukio hilo limefanyika jana hii katika Ofisi za DickSound Mall maeneo ya Magomeni Dar es salaam ambapo Dick amesema “Nimempa kama zawadi siyo kwa ajili ya Ubalozi, alikuja kwangu wakati anaenda kupambana nikamuahidi akishinda nitaweza kumpa gari,”

“Wakati akiwa Kenya nikaona video nikamtumia kumwambia umeniangusha ushapigwa, akasema hapana sio kweli Mimi ndio napanda kupambana, hivyo leo tumemkabidhi kumpongeza na kutimiza ahadi”

Kwa upande wa Mandonga “Namshukuru sana DickSound Kwa hili leo ndoto yangu imetimia, Mandonga anaondoka na usafiri Mungu mkubwa”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live