Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mandonga atua Kenya na 'Ngumi Sugunyoo'

Mandonga Mklll.jpeg Karim Mandonga

Thu, 12 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

BONDIA mcheshi nchini Karim Mandonga maarufu kama ‘Mtu Kazi’ amempiga mkwara mzito mpinzani wake Daniel Wanyonyi raia wa Kenya kwamba amekwenda na ngumi ya kigeni iliyozaliwa Ukraine kwenye midundo ya mabomu. Ngumi inayoitwa Sugunyoo.

Mandonga ametoa kauli hiyo leo tarehe 12 Januari, 2023 wakati akizungumza na waandishi wa habari nchini Kenya kuhusu pambano hilo linalotarajiwa kufanyika katika ukumbi wa KICC Jumamosi nchini humo.

Bondi huyo aliwasili nchini Kenya jana tarehe 11 Januari, 2023 kwa ajili ya maandalizi ya pambano hilo dhidi ya Wanyonyi linalosubiriwa kwa hamu

“Wanyonyi lazima tukupige tu! Unataka tunakupiga, hutaki tunakupiga! Hapa hapa Kenya,” amewaambia wanahabari.

Mandonga amebainisha kuwa yuko nchini humo kwa kubwa ya kumchapa mpinzani wake na baadaye anaweza kuchukua muda wa kubarizi.

“Toka nianze mchezo wangu wa Boxing, sijawahi kuahidi kwamba bondia nitampiga katika raundi ya ngapi, ila lazima apigike tu,” alisema.

Bondia huyo mwenye mbwembwe nyingi aliweka wazi kwamba yuko tayari kwa pambano lake dhidi ya Wanyonyi. Alimuonya mpinzani wa Kenya kuwa tayari kushindwa.

“Nimekuja na ngumi ya kigeni, ngumi iliyozaliwa Ukraine kwenye midundo ya mabomu. Ngumi inaitwa Sugunyoo,” alisema.

Mandonga amewashukuru mashabiki wake wa Kenya na wa Tanzania na kuwahakikishia ushindi katika pambano hilo la Jumamosi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live