Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mandonga atoa siri, kazi wanayo

C8f8e054 5d48 4601 9bf5 0beaf17cbb65 Mandonga ameshinda pambano lake la mwisho Jijini Arusha

Thu, 29 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Karim ‘Mandonga’ Said akifichua siri ya ushindi mfululizo, Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC) imesema kufutwa kwa pambano la ‘dabi’ la Mfaume Mfaume na Iddi Pialali ni kwa kikanuni na sheria na si kama Mfaume alicheza rafu.

Mabondia hao walizichapa usiku wa kuamkia juzi jijini Arusha, pambano lililotanguliwa na mengine 10, likiwamo la Mandonga aliyemchapa kwa pointi, Alibaba Tarimo kwenye uzani wa middle, raundi nne.

“Nimebadili ratiba yangu ya mazoezi, mwanzo sikuwa na ratiba inayoeleweka, lakini sasa niko makini na maandalizi yangu, najifua kwa ushindi tu na si vinginevyo” alisema Mandonga jana.

Kuhusu kumchapa kibao mpinzani wake, Mandonga alisema ilikuwa ni katika majibizano baada ya kuambiwa ajiandae kwa kipigo na achague ‘azikwe’ Dar es Salaam au Arusha.

“Mpinzani wangu alinitambia akidai lazima ‘nife’ kwa kipigo, nikamwambia haniwezi, nitampiga nje ya ulingo na ndani ya ulingo, katika majibizano ya kimchezo ndipo nikamchapa kibao, ingawa kile nilichomwambia ndicho kimetokea,” alijinasibu Mandonga.

Siku hiyo, pambano kuu la dabi ya Manzese na Mabibo, zilitoka suluhu baada ya bingwa kutopatikana kufuatia pambano hilo kufutwa.

Hata hivyo, kambi ya Idd Pialali inaamini Mfaume Mfaume alicheza faulo baada ya kuzidiwa na mpinzani wake, ingawa TPBRC imesisitiza pambano hilo litarudiwa.

TPBRC imekwenda mbali zaidi na kueleza kwamba, mabondia hao waligongana katikati ya mchezo, na Pialali kuathirika zaidi, lakini si kama Mfaume alicheza faulo ya makusudi.

“Kwa kuwa haikuwa imefika raundi ya nne, pale hakuna bingwa, ili kumaliza ubishi, wataandaliwa pambano la marudiano,” alisema Katibu mkuu wa TPBRC, Yahaya Poli.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live