Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mandonga apigwa tena

Mandonga Muller Mandonga apigwa tena

Mon, 28 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia Muller Jr ameibuka mshindi kwenye pambano la Raundi Sita dhidi ya Karim Mandonga pambano la Tamasha la Uzinduzi wa Mchezo wa Ngumi Zanzibar lilopigwa katika uwanja wa Mao Tse Tung, Zanzibar.

Muller Jr ameshinda kwa uamuzi wa Majaji na kuwa moja ya walioandika historia ya kushiriki kwenye tukio la kuurejesha tena mchezo wa Masumbwi Zanzibar baada ya miaka 60 kupita bila ya mchezo huo.

Pambano hilo la Raundi Sita limeshuhudiwa na Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi ambaye alijuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa mashindano ya ngumi yaliyopigwa marufuku Kisiwani hapo zaidi ya mika 50 iliyopita ambapo Majaji wote watatu wamempa ushindi Kiluwa kwa pointi 55-56, 56-58 na 55-59

Hii ni mara ya tatu mfululizo Mandonga kupigwa. Julai 22 alipoteza pambano la marudiano na Mkenya Daniel Wanyonyi, na Julai 29 alipoteza pambano dhidi ya mganda Moses Golola na sasa Mandonga anasema anajipanga kwa ajili ya pambano jingine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live