Bondia Mtanzania, Karim Mandonga ‘Mtu Kazi’ amempiga bondia Mkenya Daniel Wanyonyi kwa mtoano wa kiufundi (TKO) raundi ya sita katika pambano la raundi 10 lisilo la ubingwa, la uzani wa ‘Super Middle’ kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Kenyatta (KICC) nchini Kenya usiku wa kuamkia leo.
Mandonga mtu kazi, mwenye uzani wa kilo 83.5 alivalia uzi wa rangi ya samawati nae Wanyonyi atavalia rangi nyekundu akiwa na kilo 80.2.
Majaji Kwenye pambano hilo la kukata na shoka walikuwa ni Franklyn Imbenzi , Charles Juma na Leonard Wanga. Mwamuzi wa kati alikuwa Julias Odhiambo.
Bondia wa Tanzania Mandonga Mtu Kazi ambaye alipata umaarufu katikati ya mwaka jana kutokana na kutamba kwake kisha kupigwa, qmekuwa ni mfano wa jinsi masoko yanavyoweza kufanya bidhaa kutamanika.
Misemo yake ya ubunifu imempa umaarufu zaidi kuliko bondia Mkenya Wanyonyi ambaye ameshinda mataji mengi zaidi. Jina la pili la Karim Mandonga ni kujiamini.