Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mandonga amtangazia vita Mada Maugo

Mandonga Pic Mandonga amtangazia vita Mada Maugo

Tue, 12 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia wa ngumi za kulipwa Karim Mandonga ‘Mtu Kazi’ amemchokonoa Bondia mkongwe nchini, Mada Maugo kwa kumwambia kuwa hata iweje haitokuja kutokea yeye kupigwa na bondia huyo na kama ataendelea kumleta kiburi basi akamuulize jirani yake Said Mbelwa alichofanyiwa Morogoro.

Mandonga amesema kuwa yeye hawezi kumuogopa Mada Maugo kwa kuwa ngumi ndiyo kazi yake hivyo hawezi kukubali kupigwa na bondia huyo ambaye tayari ameshamchapa jirani yake.

“Nikwambie Mandonga ‘Mtu Kazi’ hawezi kupigwa na bondia mlevi (Mada Maugo), nafanya mazoezi ya kutosha na nipo sawa hivyo akija au atafute promota aone nitakavyompoteza kwa sababu siwezi kupigwa kijinga na huyo,” amesema Mandonga.

“Mada Maugo amekuwa akiongea sana, anataka nimchape kama nilivyofanya kwa jirani yake Said Mbelwa nilivyompiga pale Morogoro, nataka niwaambie Maugo sasa hakuna bondia, amebakia mdomo peke yake.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live